Diamond Platnumz. MOJA ya tatizo kubwa la kitaifa ambalo Watanzania tunalo ni kukosa uzalendo, sumu hiyo ilianza kututafuna taratibu na sasa inazidi kukua katika maeneo mengi.
Ukitaka kuamini tazama jinsi wacheza soka wanavyocheza wakiwa timu za taifa, angalia baadhi ya viongozi wa siasa na serikalini wanavyofanya ufisadi kwenye mali za uma bila hata aibu.
Msanii wa Kitanzania, Diamond Platnumz ni mmoja wa wanaowania Tuzo za MTV Mama 2015, inaeleweka wazi kuwa hakuna anayelazimishwa kumshabikia msanii fulani lakini kumekuwa na idadi kubwa ya Watanzania wanaojitokeza na kumpinga Diamond kimataifa huku wakimuunga mkono Davido wa Nigeria.
Licha ya Diamond kufanya kazi na wasanii wa Nigeria lakini hakuna mashabiki wa Nigeria wanaojitokeza na kutangaza kimataifa kumuunga mkono Diamond katika tuzo hizo, hiyo inaonyesha jinsi ambavyo uzalendo wa Watanzania unavyoelekea shimoni.
Kupingana kushabikiana mara nyingi kunatakiwa kuishie ndani ya nchi lakini Watanzania wenzetu wanapovuka mipaka kisha kutumia nguvu kubwa kuwaponda na kuonekana hawafai ni sawa na kujimaliza wenyewe.
Hivi karibuni Davido kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Instagram, aliandika ujumbe wa kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura lakini akasema hataki kura zetu bali anataka Watanzania wampigie kura Diamond na hataki usumbufu kwenye ukurasa wake.
Inawezekana likaonekana ni jambo la kawaida lakini kauli kama hiyo ni zaidi ya aibu kwa Watanzania. Kama haumsapoti Diamond kuna haja gani ya kutangaza kimataifa kuwa apigiwe kura msanii wa nje ya nchi yako!
Diamond anawania tuzo katika vipengele vitatu akiwa na Mtanzania mwingine, Vanessa Mdee kwenye kipengele kimoja.
Sina maana ya kuwa lazima Watanzania wampigie kura Diamond, lakini kujitokeza ‘ki-front-front’ na kuwatangaza wa nje wakati wao hawatutangazi sisi, huu ni upuuzi. Kwa nini hatujiulizi mbona wasanii wetu hawamo wengi katika tuzo za kimataifa badala yake tuna kazi kubwa ya kuvunjana nguvu sisi kwa sisi.
Tuzo hizo ambazo zitafanyika kwa mwaka wa 10 tangu kuanzishwa kwake, zitatolewa Julai 18, 2015. Baadhi ya vipengele vipo hivi:
Msanii Bora wa Kiume
AKA (Sauz)
Davido (Nigeria)
Diamond (Tanzania)
Sarkodie (Ghana)
Wizkid (Nigeria)
Msanii Bora wa Kike
Bucie (Sauz)
Busiswa (Sauz)
Seyi Shay (Nigeria)
Vanessa Mdee (Tanzania)
Yemi Alade (Nigeria)
Kundi Bora
B4 (Angola)
Beatenberg (Sauz)
Black Motion (Sauz)
P-Square (Nigeria)
Sauti Soul (Kenya)
Msanii Bora Anayechipukia
Anna Joyce (Angola)
Cassper Nyovest (Sauz)
Duncan (Sauz)
Patoranking (Nigeria)
Stonebwoy (Ghana)
Msanii Bora wa Hip Hop
Cassper Nyovest (Sauz)
K.O. (Sauz)
Phyno (Nigeria)
Olamide (Nigeria)
Youssoupha (DRC)
Ushirikiano Bora
AKA, Burna Boy, Da LES & JR: ‘All Eyes On Me’ (SA/Nigeria)
Davido ft Uhuru & DJ Buckz: ‘The Sound’ (Nigeria/SA)
Diamond & Iyanya: ‘Bum Bum’ (Tanzania/Nigeria)
Toofan & DJ Arafat: ‘Apero Remix’ (Togo/Ivory Coast)
Stanley Enow & Sarkodie: ‘Njama Njama Cow Remix’ (Cameroon/Ghana)
Wimbo wa Mwaka
Cassper Nyovest: ‘Doc Shebeleza’ (Sauz)
Euphonik featuring Mpumi: ‘Busa’ (Sauz)
DJ Fisherman & NaakMusiQ featuring DJ Tira, Danger & Dream Team: ‘Call Out’ (Sauz)
K.O featuring Kid X: ‘Caracara’ (Sauz)
Lil Kesh Featuring Olamide & Davido: ‘Shoki Remix’ (Nigeria)
Mavins: ‘Dorobucci’ (Nigeria)
Sauti Soul: ‘Sura Yako’ (Kenya)
Toofan: ‘Gweta’ (Togo)
Wizkid: ‘Show You The Money’ (Nigeria)
Yemi Alade: ‘Johnny’ (Nigeria)
Msanii Bora kwa Kutumbuiza Live
Big Nuz (Sauz)
Diamond (Tanzania)
Flavour (Nigeria)
Mi Casa (Sauz)
Toofan (Togo)
Video ya Mwaka
‘Crazy’ – Seyi Shay Ft Wizkid; Director: Meji Alabi
‘Doors’ – Prime Circle; Director: Ryan Kruger
‘Love You Everyday’ – Bebe Cool; Director: Clarence Peters
‘Nafukwa’ – Riky Rick; Director: Adriaan Louw
‘The Sound’ – Davido Featuring Uhuru & DJ Buckz; Director: Sesan
Msanii Bora wa Pop
Fuse ODG (Ghana)
Jeremy Loops (Sauz)
Jimmy Nevis (Sauz)
Nneka (Nigeria)
Prime Circle (Sauz)
Kupiga kura, tembelea tovuti ya MTV BASE au katika kurasa zao za Facebook na Twitter.