Monday, June 15, 2015

WEMA:STAA YEYOTE NAWEZA KUTOKA NAYE

Mwadada anayefanya poa sana kwenye tasnia ya Bongo Movies, Wema Sepetu.
Makala - Bongo
Saphyna Mlawa
KATIKA orodha ya wanadada wanaofanya poa sana kwenye tasnia ya Bongo Movies, hata siku moja huwezi ukaacha kutaja jina la Malkia, Wema Sepetu ambaye alijipatia umaarufu kutokana na kazi nzuri tangu pale alipofanya muvi ya kwanza ‘The Point of No Return’ aliyoshilikishwa na marehemu Steven Kanumba na nyingine nyingi.
Hata hivyo, staa huyo ameendelea kuwa lulu kwenye fani hiyo kutokana na kujituma kwake pamoja na kufungua kipindi binafsi kinachojulikana kwa jina la ‘In My Shoes’ kinachoruka kwenye Kituo cha Televisheni cha EATV kila Jumatano.   
Pamoja na hayo, maisha ya staa huyo yamekuwa ya kubadilikabadilika kila mara, akiandamwa na vyombo vya habari, akikosana na rafiki zake na mengine mengi. Unahitaji kufahamu namna anavyokabiliana na changamoto hizo? Gazeti la Championi Jumatatu linakutiririshia sehemu ya mahojiano na diva huyo.
Vipi maendeleo ya kazi zako kwa sasa?
Maendeleo ya kazi zangu ni mazuri sana na kila kukicha napambana ili nifike mbali zaidi kwa kuandaa kazi zenye ubora za kuwabamba mashabiki wangu.

Nini sababu ya kutibuana mara kwa mara na kila rafiki unayempata?
Ha, ha, ha! Kama unamjua Wema vizuri, nadhani utakuwa na jibu la swali hilo. Mimi binafsi nimekuwa mtu wa kupenda amani na upendo mara nyingi, ila unajua nini, marafiki ninaokuwa nao ndiyo wanakuwa chanzo cha ugomvi. Kifupi ‘I hate that situation’, pia siwezi kuzingatia sana, maana ninachowaza muda mrefu ni pesa tu.
Muvi yako uliyoigiza na Van Vicker, ‘Day After Death’ itatoka lini?
Muda si mrefu nitaiachia. Mashabiki wangu wakae tayari, ‘coz for now’ kazi iko jikoni ambapo nimepanga kuifanyia uzinduzi hapa nyumbani na Ghana, japokuwa sijajua ni sehemu gani nitafanya uzinduzi huo, ila siyo muda mrefu nitawajuza watu wangu wa nguvu.

Baada ya kuachana na Diamond, je, una mpango wa kutoka na staa mwingine?
Ha! Ha! ‘Well’ siwezi kusema sitatoka na supastaa utakuwa ni uongo! Love is blindness, it comes automatically. Akitokea supastaa sina shida as long as tunaendana.

Unazungumziaje kauli ya Kajala kukuomba msamaha?
Kwa sasa sina cha kuzungumzia juu ya suala hilo, ila siwezi kusema kwamba milele sitaongea naye. Ikitokea poa, isipotokea
‘I just mind my own business’.