Monday, June 15, 2015

Ratiba ya kuaga mwili wa Marehemu Mufti Shaaban Simba pamoja na mazishi imetolewa… (Audio)

IMG-20150615-WA0020
Stori ya Msiba wa aliyekuwa Sheikh Mkuu Tanzania, Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba imechukua nafasi kubwa sana kwa kuripotiwa kwenye vyombo vingi vya Habari.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum nimemnukuu akithibitisha juu ya msiba huo >>> “Ni kweli Mheshimiwa Mufti amefariki.. Kesho saa nne asubuhi Waislamu na Viongozi wote watajumuika Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni Muslim kuuaga mwili wa Sheikh. Mchana mwili wa Sheikh utasafirishwa kwenda Shinyanga, atazikwa siku ya Alhamisi“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum
Hapa anamzungumzia Marehemu Mufti Simba>>> “Mufti alikuwa  na sifa ya kuwa Kiongozi wa Waislamu. Alikuwa mvumilivu sana na msamehevu katika Utawala wake. Angekuwa hana subira Waislamu wasingekuwa na uvumilivu“>>>– Sheikh Alhadi Mussa Salum
IMG-20150615-WA0021
Hapa nina sauti niliyomrekodi Sheikh Alhadi Mussa Salum akizungumzia msiba huo na akimzungumzia Marehemu pia.