Thursday, July 2, 2015

AUNT: NITAMSAPOTI WEMA MPAKA KIELEWEKE!

Chande Abdallah
DIVA wa filamu Bongo ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja anayetambulika kwa jina la Cookie, Aunt Ezekiel, amefungukia kuhakikisha anampa sapoti ya nguvu shosti wake, Wema Sepetu katika harakati zake za kuwania ubunge.
DIVA wa filamu Bongo ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja anayetambulika kwa jina la Cookie, Aunt Ezekiel akiwa na shogaake Wema Sepetu.
Akiwamwagia ‘ubuyu’ Amani, Aunt alidai kuwa pamoja na kwamba yeye hafahamu siasa hata kidogo na hatarajii kujiingiza huko, lakini anatambua Wema ameamua kutangaza nia ya kugombea, hivyo kama rafiki yake mkubwa atahakikisha anazunguka naye kila sehemu ili kumsaidia atimize ndoto zake za kuingia mjengoni na kuwatumikia wananchi wa Singida.
“Kama rafiki wa Wema nitahakikisha nampa sapoti ya nguvu rafiki yangu hadi aingie mjengoni, japo kuwa mimi binafsi sipendi siasa na sitaki kujiingiza huko,” alisema Aunt Ezekiel.
Wema ni mmoja kati ya wasanii waliojitokeza katika kinyang’anyiro cha kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalumu jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya CCM.