Thursday, July 2, 2015

MAJUTO ADAI KUSHOBOKEWA NA ‘VIBINTI’

Brighton Masalu
STAA mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amefungukia shutuma anazopewa na mashabiki wake kwa kupenda kuonekana na ‘vibinti’ kuwa wanamshobokea mwenyewe.
Staa mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’.
Akichezesha taya na Amani, Mzee Majuto ambaye kifani ni bingwa wa komedi alisema, kutokana na kazi yake ya uigizaji imemfanya kuzimikiwa haswa na mabinti.
“Sijawahi kumshobokea binti yoyote ila wenyewe ndiyo huwa wananishobokea kutokana na uigizaji wangu,” alisema Mzee Majuto.
Hivi karibuni, Mzee Majuto alidaiwa kuoa binti mdogo ambaye ni sawa na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18 akidai kuwa sheria ya dini inamruhusu kufunga ndoa wa wake wanne.