Saturday, July 11, 2015

BINTI AMUUA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUMLAZIMISHA KUFUA NGUO CHAFU!!

Si jambo la kawaida kusikia mtoto kamuua mama
yake ama mama kamuua mtoto wake, japo kwa
miaka ya sasa matukio kama hayo yameshamiri
kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali duniani.
Tukio la mtoto kumuua mama yake leo limechukua
headlines huko Zimbabwe baada ya kutokea
kutoelewana baina yao.
Kilichotokea ni kwamba binti wa miaka 17
amemuua mama yake kwa kumchoma moto baada
kulazimishwa kufua nguo chafu, kitendo
kilichomkasirisha na kufikia uamuzi huo.
Kabla ya kumuua mama yake kwa kumwagia
mafuta kisha kumchoma moto, mama yake
alimpiga kitendo kilichomuuzi binti huyo na
kufanya uamuzi huo mgumu.
Polisi wamemfungulia mtoto huyo mashtaka ya
mauaji licha ya kupewa taarifa kuwa alikua
akisumbuliwa na ugonjwa wa akili.