KUNDI la kigaidi la Boko Haram limeua raia 43
katika mashambulio makubwa dhidi ya vijiji vinne
vilivyoko katika jimbo la Borno lililopo kaskazini
mashariki mwa Nigeria.
Wanakijiji na polisi wamethibitisha kuwa wanakijiji
43 wameuawa jirani katika jimbo la Borno.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, wanamgambo wa
Boko Haram walivivamia vijiji hivyo ambapo
nyumba kadhaa katika vijiji hivyo zilichomwa moto
na wapiganaji hao wa Boko Haram.
Polisi ya Nigeria imetangaza kuwa bado inazifanyia
uchunguzi taarifa za kuuawa kwa raia katika
mashambulio hayo huko Borno.
Wanamgambo wa Boko Haram wameendelea
kufanya mauaji dhidi ya raia nchini Nigeria na
katika nchi za jirani na hivyo kuzidi kuipa
changamoto serikali mpya ya nchi hiyo chini ya
Rais Muhammadu Buhari.
Rais Buhari aliyeingia madarakani mwishoni mwa
mwezi Mei mwaka huu anakabiliwa na mashinikizo
makubwa baada ya kundi la kigaidi la Boko Haram
kuzidisha mashambulizi yake dhidi ya raia katika
mwezi huu mtukufu wa Ramadhani hasa maeneo
ya kaskazini mwa Nigeria.