Sunday, July 12, 2015

MAIMARTHA ALA SHAVU AZAM TV!

Mtangazaji maarufu nchini, Maimartha Jesse juzi kati alilamba shavu la kutangaza Azam Tv na kufanikiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema anafuraha tele kupata shavu hilo kwani alikuwa akilisubiria kwa hamu na amejiona ni mwenye bahati kubwa kwani wapo watangazaji wengi lakini limemuangukia yeye.
“Yaani watu wangu wakae mkao wa kula kwani hili shavu nililopata safari hii litanifanya nifanikishe mambo mengi ambayo yalikuwa yamelala, kipindi changu kitawafaidisha wasanii wengi kwani kimejipanga vizuri na kinaitwa Muziki Mtamu,” alisema Mai.