Wednesday, July 15, 2015

MSANII ADAI KUTOA MIMBA YA ALI KIBA

Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amedai licha ya kutembea na wasanii wengi, aliwahi kupata ujauzito wa mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba lakini kwa bahati mbaya, ikatoka, Risasi Mchanganyiko lina ‘full details’.
moreStaa wa Bongo Fleva, Ali Kiba.
Akifunguka bila wasiwasi mbele ya kamera na masikio ya waandishi, msanii huyo anayetambulika mtaani na filamu za Gundu na Judgement Day, aliwataja wasanii ambao alishiriki nao mapenzi na kuelezea pia wasifu wao.
“Nilikuwa nikifahamika hadi nyumbani kwao Kariakoo. Mama yake alinipenda sana kwani kila baada ya siku kadhaa nilikuwa nikienda kushinda kwao sambamba na kupika na yeye (Ali Kiba) alikuwa akija kwangu usiku tunalala wote.
 “Nilimuamini sana Ali kiasi cha kutoka naye kimapenzi bila kutumia kinga hadi kufikia kushika mimba yake.
BOZIGLOBALTVONLINE4Lakini mimba ilitoka kwa bahati mbaya ikiwa na miezi miwili tu,” alisema Bozi.
Msanii huyo alienda mbali zaidi na kuwataja wasanii wengine aliotembea nao kuwa ni pamoja na Nay wa Mitego ambaye hakudumu naye, Dogo Aslay, Bob Junior na wengine wengi.
“Kila mmoja alikuwa na muda wake, wala sikuwa nawapanga kwa kipindi kimoja. Nikiachana na huyu nakuwa na huyu. Kila mmoja alikuwa akinivutia kitandani lakini kwa Bob Junior alikuwa zaidi ya wote.”
Baada ya madai yote haya kutoka kwa msanii huyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumtafuta Ali Kiba kwa njia ya simu kuweka wazi juu ya kumpachika mimba msanii huyo ambapo alifunguka;
“Huyo msichana namjua, ila naona anatafuta maneno kwani anachoongea siyo kweli. Anatafuta kiki tu.”