Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefungua mlango kwa mwanaume yoyote anayetaka kumuoa ajitokeze ilimradi awe na vigezo 10 ambavyo ameviainisha.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C ameandika:
“Habari zenu wapendwa wote dunia nzima!Leo na habari nzuri sana kwenu,Naomba kuwatangazia kuwa natafuta Mchumba wa kuishi nae milele!nataka niwe nae milele na nimzalie watoto wawili wa kike na wakiume!!!!
Ila naomba niwambie kabisa masharti
1.Awe mpole ili nikikasirika anibembeleze
2.Awe anapenda muvi za kihindi ili nikiwa na stress aniwekee nyimbo za kihindi maana ndio raha ya moyo wangu.
3.Asiwe muongeaji sana sababu huwa sipendi makelele.
4 Anipende na ubonge wangu huu asije akaanza kunambia baby anza mazoezi au dah baby zamani ulikuwa bomba au rudisha kiuno hapo hatutaelewana.
5.Awe ananipikia nikichoka maana navutiwa nikimuona mwanaume anapika.
6.Awe na Mimi muda wote maana na wivu sana ikiwezekana tufanye kazi ofisi moja au awe ofisi ijengwe hapo hapo nyumbani.
7.Awe mvumilivu maana nikiwa na hasira huwa naongea kwa sauti ya juu sana.
8.Asiwe na rafiki wengi,na akitaka kuonana nae na mi niwepo maana si mnajua wanaume tena wakikutana huwa wanashaurina mabaya.
9.Awe anajua nyimbo zangu zote ndio ntaamini kweli ananipenda.
10.Sharti la mwisho kabisa ambalo ni muhimu sana kwangu ni hili tuwe tunatumia simu moja na Namba moja, maana kanisani tunafundishwa kuwa ndoa maana yake tumeungana na kuwa kitu kimoja kwahiyo kama mume na mke tunalala pamoja kitanda kimoja na kuishi pamoja kwanini tusitumie simu moja!Sioni tatizo!Kama una ndugu,jamaa.kaka,rafiki yuko single basi mjulishe tangazo hili huezi jua unaeza ukashangaa nimekuwa shemeji yako au wifi yako”.