Thursday, July 2, 2015

HOFU MTOTO WA ZARI KUFIA TUMBONI

zariMpenzi wa sasa wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ .
STORI: MWANDISHI WETU
HABARI ya mjini kwa sasa ni mjadala mzito mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba, mpenzi wa sasa wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anaweza kumuua motto aliye tumboni kutokana na tabia yake ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu (high hills) katika kipindi hiki cha ujauzito.
PhotoGrid_1429005202683Diamond Platnumz akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.
WALICHOKISEMA MASHABIKI
Baadhi ya mashabiki, hasa watoto wa mjini wanaosadikiwa kuwa na mapenzi makubwa na Miss Tanzania 2006 aliye pia nyota wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu (Team Wema), ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond, wamemnanga Zari wakisema kuvaa kwake high hills ‘kokoko’ kunaweza kumminya tumbo wakati wa kutembea hivyo kukifanya kitoto hicho kufia tumboni.
DOKTA AZUNGUMZA, AFAFANUA
Kufuatia madai hayo mazito, juzi Amani lilizungumza na daktari maarufu jijini Dar, Godfrey Chale ‘Dokta Chale’ ambaye alilazimika kueleza kuhusu madai hayo.
Amani: “Samahani dokta, tumelazimika kukutafuta kutokana na maneno yaliyosambaa kwa sasa hapa mjini. Diamond ana mpenzi wake ni mjamzito. Sasa pamoja na ujauzito wake, anavaa viatu virefu.
“Kwa hiyo wanamnanga kwamba anaweza kukiua kitoto kilichopo tumboni kwa sababu anapovaa viatu hivyo, misuli ya
miguu inakaza na anabana tumbo. Kuna ukweli?”
Dokta: “Kwanza kabisa siyo kweli. Mwanamke anapovaa viatu virefu wakati wa ujauzito hakusababishi mtoto tumboni kufa.
“Ila, inashauriwa wajawazito
wasiwe wanavaa viatu virefu kwa sababu, wanapovaa, wanatanua misuli na kujiongezea uzito. Kwa hiyo inakuwa kama mtu aliyebeba mzigo kichwani huku akiwa na mimba.”
ATAJA MAGONJWA YANAYOMKABILI ZARI
Dokta Chale aliendelea kuweka wazi kuwa, mjamzito anapopendelea kuvaa viatu virefu, akishajifungua na mwili ukapoa, atakabiliwa na magonjwa manne.
“Kwanza ataugua miguu. Pili, atasumbuliwa na matatizo kwenye visigino. Tatu atapata matatizo ya magoti na nne ataugua mgongo. Ndiyo maana unaweza kukuta mwanamke anakuwa mrembo, miguu mizuri lakini kama alikuwa akibeba mizigo au kuvaa viatu virefu wakati wa mimba, miguu inaota nyama kwa nyuma ‘kiazi’.”
AONDOA HOFU
“Kwa hiyo, kama jamii ina hofu kwamba huyo mjamzito atamuua mtoto aliye tumboni kwa sababu ya kuvaa viatu virefu, hofu hiyo iondoke bali yazingatiwe hayo matatizo manne niliyoyasema,” alisema daktari huyo.
KWA WANAWAKE WOTE
“Lakini madhara haya si kwa wajawazito tu. Utafiti wa kitaalam umegundua kuwa, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku. Kwa hiyo kuvaa viatu vyenye visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa zaidi. Sasa utaona madhara ya kutembea hatua 10,000. Hii haijalishi anayetumia gari.
“Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya kwenye miguu, kiuno, mgongo na shingoni kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito. Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino,” alimalizia dokta huyo.
DIAMOND ALIVYOSEMA
Amani, juzi lilimtafuta Diamond kwa njia ya mtandao wake wa WhatsApp na kumuuliza anachukuliaje madai ya ‘wabaya’ wa Zari:
“Hao wapo tu. Unajua dunia hii ukishakuwa maarufu kila jambo litakuandama. Lakini mimi naangalia mbele zaidi, nini nafanya na nini nitafanya. Kama maneno hata kwenye kanga yapo.”