Thursday, July 2, 2015

WASTARA: NAMPA BOND NAFASI YA KUNIOA

WASTARA Juma Issa Abeid amekiri kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na ukweli kwamba damu yake bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki huku akimpa nafasi kubwa msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi vigezo na masharti.
Wastara Juma Issa Abeid akiwa na Bond.
Akifungulia ‘koki’ ya maneno mbele ya paparazi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Wastara ambaye kwa sasa yuko bize kusaka ubunge nyumbani kwao Morogoro Vijijini, alisema hawezi kudanganya kwamba ataishi bila kuwa na mume kwa kuwa amekamilika kimaumbile.
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji ananitamani tu.
“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.