Thursday, July 2, 2015

RICK ROSS AACHIWA KWA DHAMANA YA DOLA MILIONI MBILI

Rapa maarufu duniani anayetokea nchi ya Marekani, Rick Ross.
Rick Ross alipokuwa gerezani.
MWANAMUZIKI Rick Ross wa Marekani ameachiwa huru baada ya kuweka dhamana ya dola milioni mbili kutokana na kutiwa mbaroni Juni 24 mwaka huu kwa tuhuma za kumteka nyara na kumshambulia mlinzi wake na kumtishia kwa bastola.
Rapa huyo pia ameweka dhamana jumba lake lilikoko Fayette, Jimbo la Georgia, ambalo lilikuwa likimilikiwa na bondia Evander Holyfield.
NA MTANDAO WA NAIJA GIST