Jana tuliipata taarifa ya kushtua, ilikuwa msiba wa Mwanamuziki ambae kwa Tanzania alikuwa Legend kwenye muziki wa Dansi, Ramadhan Masanja aka Banza Stone… Sauti yake iliwahi kusikika kwenye bendi chache ikiwemo hizi mbili kubwa za Tanzania, African Stars ‘Twanga Pepeta‘ na TOT Plus iliyokuwa inaongozwa na Marehemu Kapteni John Komba.
Leo watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao Sinza, kwa ajili ya kumuaga na kumsindikiza Banza Stone kwenye safari yake ya mwisho duniani.
Mazishi yamefanyika kwenye Makaburi ya Sinza Dar es Salaam.
RIP Banza Stone, safari yake Duniani itakumbukwa kwa mengi lakini hasahasa ni kazi ya muziki mzuri wenye ujumbe ambao japo leo hatuko nae lakini muziki na ujumbe wake utaishi milele !!
Hii ni moja ya kazi nzuri ambazo na yeye alikuwepo ndani, inaitwa ‘MTU PESA’-AFRICAN STARS (Twanga Pepeta)