Thursday, August 13, 2015

BREAKING NEWS : MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA AHAMIA CHADEMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ametangaza rasmi kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivi punde.
Mgeja ametangaza uamuzi huo wakati akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo ametumia kauli ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 alipozungumzia haja ya chama hicho kujisahihisha kwamba "Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.”