Thursday, August 13, 2015

Diamond: Nipo tayari kwa kifo!

diamond mtotoStaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mtoto wake Latifah ‘Princess Tiffah’.
SIKU chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kupata binti na kumwita Latifah ‘Princess Tiffah’ na kuanza maisha mapya ya familia na mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’, nyota huyo anadaiwa kutoa ya moyoni kwa kusema kuwa sasa yupo tayari kwa kifo kwa vile ndoto yake kubwa ya kupata mtoto imekamilika na ana chata duniani.

A photo posted by Tiffah Dangote👸 (@princess_tiffah) on 
KWANZA ANAMSHUKURU MUNGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumtimizia ndoto yake ambayo amekuwa akiiota usiku na mchana na kwa miaka mingi tangu kuingia ‘ukubwani’ hivyo, bahati mbaya yoyote ikitokea akapoteza uhai itakuwa poa tu kwake.
NDICHO KITU ALICHOBAKIZA
Chanzo kilikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa kuhusu mafanikio ya kimuziki na kimaisha, nyota huyo anaamini alishafikia malengo, alibakiza kimoja tu, mtoto.
“Unajua katika maisha, ukipata mali au mafanikio mengine ujue tatizo kubwa litabaki kwenye familia na familia yenyewe si kupata mke au mume bali kupata mtoto.
“Sasa jamaa siku zote alikuwa akisema, pesa kwake si tatizo, nyumba ya kuishi nzuri anayo, gari la kutembelea pia. Kilichokuwa kikiuchakaza moyo wake ni kutopata mtoto ili awe kama wengine. Hicho ndicho kitu alichokuwa amebakiza hapa duniani,” kilisema chanzo.
ZARI NAYE HANA FURAHA YA MTOTO
Chanzo kikazidi kudai kuwa, wakati Diamond akifurika machozi ya furaha kwa kupata mtoto, mzazi mwenziye, Zari yeye hana furaha kufuatia baba wa watoto wake watatu au aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga kumpiga madongo kupitia mtandao wake wa Instagram.
Mfano, juzi kwenye mtandao wake, jamaa huyo ametupia picha akiwa na mtu anayedaiwa kuwa eti, ndiye baba wa mtoto Tiffah.
“Zari anaujua ukweli kwamba mtoto ni wa Diamond. Sasa wale jamaa kuendelea kutangaza si wa Diamond wao wanajuaje wakati siri ya mtoto ni wa nani anaijua mama? Hayo ndiyo maneno ya Zari kila kukicha.
“Yeye ni mtu mzima, ana akili timamu. Hawezi mtoto wa huyu akampa yule. Nadhani maneno ya aliyekuwa mumewe ndiyo yanamkosesha raha. Lakini Diamond mwenyewe ni peace tu.” Chanzo.
Baada ya kujazwa ubuyu huo, paparazi wetu alifanikiwa kukutana uso kwa macho na Diamond mwenyewe ambaye kweli alionekana mwenye furaha muda wote na hata alipogusiwa hilo alimshukuru Mungu akisema maombi yake yamekubaliwa.
STUDIO YA DIAMOND HAIKALIKI
Habari zaidi zinasema kuwa, nyota huyo kupata mtoto imekuwa ‘nongwa, watu hawali wala hawanywi’. Hapatikani kwenye studio yake ya Wasafi Record iliyopo Sinza Mapambano.
Amani lilifika juzi na kumkosa lakini mmoja wa wafanyakazi wake alisema: “Weee! Chezea kichanga wewe. Baba Tiffah anakuja lakini si kama zamani. Unajua kwa sasa muda mwingi yupo na mwanaye.”
MSIKILIZE
Baadaye Amani lilimpata Diamond kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alisema: “Kusema kweli namshukuru Mungu kwa kila jambo ila zaidi kunipatia huyu Princess Tiffah. Kwani uwepo wake ni furaha kwangu na ni historia kubwa katika maisha yangu.
“Leo hii ikitokea nikafa basi watu watanikumbuka zaidi wakimuona mwanangu, maana huyo ndiye mrithi wa kila kitu kwangu.“Nilikuwa najiuliza nikifa sina mtoto itakuaje? Ina maana sitaacha kumbukumbu. Lakini kwa sasa nipo tayari kwa kifo kama Mungu amenia-ndikia.