Monday, August 24, 2015

DIANA KIMARO CHUPUCHUPU KUBAKWA

 Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’
Kisa pombe! Habari ya kushtua inaeleza kwamba, mwigizaji katika tasnia ya filamu Bongo, Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’ amekiri kunusurika kubakwa na msanii mwenye hadhi na ‘taito’ kubwa katika gemu la sanaa Bongo (hakumtaja), chanzo kikiwa ni ulabu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda jijini Dar, wikiendi iliyopita, Diana alifunguka kuwa, tukio hilo lilijiri maeneo ya Ilala, Dar hivi karibuni baada ya msanii huyo kutaka kumbaka na kusababisha kususia kwa muda masuala ya uigizaji kabla ya kushawishiwa tena na baadhi ya wasanii wenzake.
Elizabeth Michael akiwa na Diana Kimaro (kulia). 
“Tulikuwa kambini, tukawa tumekunywa sana, jamaa alikuwa akinitaka kwa muda mrefu hivyo akawa ananilazimisha nikamkatalia, muda wa kulala ulipowadia, aliingia chumbani kwangu na kulazimisha kunibaka, nilipiga kelele na kusaidiwa na mmoja wa wasanii wenzangu. Ukweli kama siyo kupiga kelele angenibaka maana alikuwa tayari ameshanizidi nguvu,” alisema Diana.