Aliyekuwa winga mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling ambaye kwa hivi sasa anaitumikia klabu ya Manchester City baada ya kujiunga nayo msimu huu akitokeaLiverpool kwa ada ya pound milioni 49. Ila headlines ni hii hapa ambapo ameamua kuuza nyumba yake ya kifahara iliyopo Southport kwa pound milioni 1.5.
Nyumba ya Sterling ambayo ina kila kitu kama ambavyo huwa nyumba za mastaa wengine wa soka duniani, Sterling anauza nyuma hiyo ikiwa ni siku kadhaa tu toka aingize kiasi kingine cha fedha baada ya kusajiliwa na klabu ya Man City. Nyumba hiyo ina vyumba vinne vya kulala, Saloon, ukumbi wa Cinema wa nyumbani, bwawa la kuogelea,Gym, Bar iliyojengwa kwa kumbukumbu ya Michael Jackson na DJ Deck zikiwa ndani yake.
Hizi ni picha zingine za jumba hilo