Msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga amefunguka kuwa, kuna mmoja wa wagombea udiwani katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar, (jina linahifadhi kwa sasa) amekuwa akimsumbua kila siku akitaka ampe penzi.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Lungi alisema mwanasiasa huyo amekuwa na tabia ya kuwarubuni mastaa wa kike na hivi karibuni alishangaa akimpigia simu na kumtaka wakutane.
“Mimi nilishangaa aliponipigia simu usiku na kuniambia ana shida ya kuonana na mimi. Sikujua alipata namba yangu kwa nani ila kwa kuwa namjua ni mpenda totoz, nilimwambia haitawezekana.
“Kuanzia siku hiyo imekuwa ni usumbufu tu, nimefikia hatua ya kufunguka ili kama anasoma hili gazeti ajue akiendelea nitamuanika, sipendi kusumbuliwa kwa kuwa nina mtu wangu anayeniweka mjini,” alisema Lungi.