Saturday, August 15, 2015

SENTESI 6 KUHUSU MSAFARA WA LOWASA ULIOZUIWA KILIMANJARO NA POLISI KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI

Lowassa Moshi 1Mchana wa August 13 2015 taarifa zinatoka kwamba Msafara wa mgombea Urais wa Tanzania 2015 kupitia UKAWA Edward Lowassa umezuiwa na Polisi kwenda kwenye mazishi ya mzee Kisumo huko Mwanga Kilimanjaro ambapo baada ya kuzuiwa waligeuza kurudi walikotoka.

 Yafuatayo ni mambo sita ambayo yametoka kwenye kauli ya Polisi Kilimanjaro kupitia kwa kamanda wake Felgensi Ngonyani mbele ya Waandishi wa habari leo August 14 2015.
 1. Tarehe 13 August 2015 Usangi wilaya ya Mwanga, katika mazishi yale kulikua na taarifa mbalimbali kwamba viongozi mbaimbali wangehudhuria akiwemo Rais Jakaya Kikwete na baadae tulipata tetesi kwamba na Edward Lowassa naye angehudhuria.
 2. Kweli siku husika tukapata taarifa za msafara wa Edward Lowassa ulipopita Mwanga mjini, nikapata taarifa kutoka kwa mkuu wa Upelelezi Mwanga kwamba msafara wa Lowassa ukiwa na magari zaidi ya 70 na pikipiki zaidi 600 wanataka kuja kwenye msiba, mimi nilikua kwenye msiba na nikaona wingi huo wa magari na pikipiki kusingepatikana sehemu ya maegesho.
 Lowassa kwenye gari3. Baada ya hapo nikawapigia simu Mh. Ndesamburo na James Mbatia ambao nao walidai wamezuiliwa wasiende kwenye mazishi Usangi, nikaongea nao nikawambia hali halisi ya huku nikaona ni busara magari ya viongozi yaani kina Mbatia, wasaidizi wao na walinzi waruhusiwe lakini sio msafara wa magari mengine na pikipiki.
 4.Baada ya kuwapa taarifa hiyo wale viongozi walikataa kwa kusema hawawezi kwenda peke yao bia Wafuasi wao, wakaamua warudi walikotoka.
 5. Baadae kukawa na taarifa kwenye mitandao kwamba nimeongea na Waandishi kwamba kuzuiwa kwa msafara ule kulitokana na shinikizo la viongozi wa ngazi ya juu na kwamba Polisi tunaonewa ile sio matashi yetu, hiyo ni uzushi na sikuongea jana na Waandishi wahabari.
 Lowassa Moshi 26. Baada ya msafara kuzuiwa kwenda msibani wakaondoka Mwanga na walipofika njia panda ya Himo wakaweka kituo kwa nia ya kutaka kufanya mkutano wa hadhara wakapaki barabarani na kuziba njia kila kona, Polisi ilibidi wapige bomu ili kutawanya ule umati ili watu waweze kupita na kuendelea na shughuli za kawaida.