Thursday, August 20, 2015

SHILOLE: NIKIIBA MUME WA MTU NISILAUMIWE

shilole.JPGMwanamuziki wa miondoko ya mduara ambaye kwa hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kilichotolewa na  Baraza la Sanaa Basata  ya kutojihusisha na shughuli za kisanaa mpaka mwaka mmoja, kitu ambacho kimemuumiza sana na kudai kuwa akiiba mume wa mtu atakuwa anakosea pia!

Akizungumza na paparazi wetu, Shilole alisema kuwa adhabu aliyopewa ni kubwa mno kiasi ambacho  anashindwa kuelewa kwa kuwa sanaa ndiyo kazi inayompatia kula na hata kuwasomesha watoto wake hivyo kumfungia mwaka mzima ni kama kumtuma kutembea hata na waume za watu  ili maisha yake yazidi kusonga mbele.

“ Mimi naona sasa wananituma kuanza kusaka waume za watu kwa kweli kwa sababu mwaka mzima kweli na ni kazi ambayo naitegemea kwa kila kitu katika maisha yangu kwa nini  mtu usiwaze vitu vingine kama huna kazi ya kufanya jamani, yaani inaniuma sana,” alisema Shilole.