Kingwendu akikabidhiwa fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kisalawe kwa tiketi ya CUF.
Katika hali ya kuonyesha kuwa UKAWA imedhamiria kushika dola, mgombea wa ubunge jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya Chama Cha wananchi (CUF), Rashid Mwinshehe 'Kingwendu' jana amechukua fomu ya ubunge na kuahidi kuwa muda wa kwenda kubutua mijicho yake na kutoa ulimi nje umewadia, huu ndio muda wa heno heno.