Monday, September 7, 2015

DIAMOND Na huyu Mtoto wawa GUMZO

Mkali wao kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mtoto wa dada yake Esma, Taraj wamezua gumzo la aina yake baada picha yao kutupiwa mtandaoni na watu kudhani ni yule Tiffah wa Diamond ambaye hajawahi kuonekana sura.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mtoto wa dada yake Esma, Taraj.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Esma kuiweka picha inayomuonesha Diamond akiwa amelala kitandani na Tahaj ndipo watu walipofikiri ni ya Tiffah na kuanza kuijadili huku wengine wakitumiana kwenye simu zao wakijulishana kuwa hatimaye ‘Tiffah’ ameonekana sura.
Kutona na gumzo kuzidi kukua kwa kasi, sosi mmoja alimpigia simu mwandishi wetu na kumtumia picha hiyo akimwambia ajionee Tiffah ameonekana sura.
“Mlikuwa mnahangaika kuipata sura ya Tiffah, huyo hapo sasa muangalie amwenyewe,” alisema sosi huyo.
Hata hivyo, mwanahabari wetu alijiridhisha kuwa mtoto huyo si Tiffah bali  Taraj wa dada yake Diamond baada ya kuwasiliana na Esma mwenyewe.