Tuesday, September 8, 2015

‘ELFU 60 TU ZINANIPELEKA KABURINI’

MGONJWAAAA (2)-001
Emakulata John akiugulia.
Aeleza alivyoanza kuugua hadi alipo sasa Na Haruni Sanchawa MWANAMKE mmoja, Emakulata John, 28, amekuwa akiugua kwa miaka zaidi ya kumi bila msaada wowote wa uhakika wa kitabibu na hali yake kwa sasa ni mbaya, hivyo kuwalilia Watanzania ili waweze kuokoa maisha yake.MGONJWAAAA (3)-001
Hivi sasa Emakulata hasikii, haoni vizuri wala hawezi  kutembea kutokana na maradhi yaliyomuandama kwa kipindi kirefu sasa na kusababishia kuwa ni mtu anayeshinda kitandani kutokana na kile alichodai kuwa mwanzo alitakiwa alipie gharama za tiba zilizogharimu Sh. 60,000 lakini akawa hana. Mgonjwa huyo hasikii na ili uweze kufanya naye  mawasilinao ni lazima umwandikie kwenye karatasi aisome kisha aanze kukuelezea hali ambayo ni ngumu sana katika maisha ya mwanadamu kama msichana huyo anavyoishi.MGONJWAAAA (4)-001
Akisimulia yaliyomsibu Emakulata anasema:
“Kwa sasa naishi na mtoto wa dada yangu karibu na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo Gongo la Mboto. Nimezaliwa miaka 28 iliyopita na kuanza shule hadi kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kigoma iliyopo mkoani Kigoma mwaka 2004, nilikuja Dar es Salaam na kufikia Ubungo na kuanza kozi ya kompyuta.”
MGONJWAAAA (1)-001
CHANZO CHA UGONJWA “Wakati nikiwa nasoma kompyuta ghafla nikaanza kuumwa, nilipokwenda hospitali kupimwa vipimo vikawa havioneshi nina tatizo gani. “Nikiwa naendelea na harakati za kujitibu hali ilizidi kuwa mbaya miguu ikawa mizito na kufa ganzi, mgongo ukawa unauma bila kujua tatizo, hiyo ilikuwa kabla ya mwaka 2004.
“Mwaka 2005 ndipo tatizo lilipojulikana baada ya kuomba msaada kwa watu nikafanyiwa vipimo tena na kuambiwa kuwa nina tatizo kwenye ubongo wa nyuma.
SH.60,000  HAKUWA NAZO
“Baada ya hali hiyo kubainika niliambiwa gharama ya matibabu na vipimo mwaka huo kwa ujumla ilikuwa Sh. 60,000 lakini nikawa sina na nilikosa msaada kutoka kwa watu ambao nilikuwa nikiwategemea.
“Kutokana na hali hiyo kuumwa nilisitisha masomo ya kompyuta ambayo nilikuwa nikisoma Ubungo jijini Dar es Salaam na kuhamia Kigamboni kwa dada yangu (jina tunahifadhi) ili niweze kupata msaada wa karibu lakini ilikuwa ni kinyume na nilivyokuwa ninategemea kwa sababu dada hakunihudumia ipasavyo. “Ubinadamu ni kazi sana (analia kisha akasitisha kuongea kwa muda wa dakika tano) nalia kwa sababu dada  yangu alinifanyia ukatili, aliniacha naumwa na nakosa usingizi kutokana na maradhi haya.
GHARAMA ZA TIBA ZAPANDA
“Baada ya kuhangaika sana mwaka jana nilipima tena kwa msaada wa watu ikabainika kuwa nina uvumbe mkubwa sana kwenye makalio kupitia uti wa mgongo na madaktari waliniambia kuwa gharama ya matibu ni Sh. 800,000 kwa kuanzia. “Sasa kama nilishindwa kulipa shilingi 60,000 hizo laki 800,000 nitazipata wapi (analia), elfu sitini tu zinanipeleka kaburini, ningekuwanazo mwanzo isingefikia gharama hii.
“Nimehangaika sana, nimetibiwa hospitali kwa misaada ya watu, nimetibiwa Bochi Medical Center iliyopo Mbezi Kwa Msuguli na kubainika kuwa nina moyo mkubwa, vifundo vimepishana na ndiyo chanzo cha kupooza.
Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane na mgonjwa huyu kwa namba ya simu 0719 464341 na mawasiliano hayo yafanywe kwa njia ya ujumbe yaani (SMS) kwani hasikii. Msichana huyo ni yatima.