Wednesday, September 9, 2015

NUH MZIWANDA: SIONI TATIZO KWA MSANII KUONESHA MAHABA KWA CHAMA ANACHOKIPENDA

Nuh Mziwanda amewataka wasanii kuwa wazalendo kwa kuonyesha hisia zao za vyama vya siasa na kuonyesha ushirikiano katika kuhamasisha.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio leo, Nuh alisema maendeleo yatakayopatikana ni manufaa kwa watanzania wote kwa ujumla.

Wewe ukiwa msanii sio kwamba sio mwananchi wa kawaida,” alisema.

Wewe pia unahitaji kutawaliwa vizuri. Unahitaji utawala mzuri ambao utaongoza hata kazi zako ziende vizuri. Kwahiyo ni vyema mtu ukajua upo upande gani. Huo ni upendo wa nchi yako na ni mzalendo. Kila binadamu anapenda uongozi mzuri ndio maana kila mtu akiwa na akili timamu ana haki ya kuchagua chama anachokitaka,” aliongeza.

Lakini sisi wasanii tusijisahau tukawa tunashindwa kuweka hisia zetu kwaajili ya maslaHi ya nchi yetu. Unaogopa kuweka wazi wewe ni chama gani, unampenda mwanasiasa gani! Sisi ni vioo vya jamii tunaangaliwa pia na watu na kuna watu wahitaji ushauri au ufafanuzi juu ya viongozi waliotangaza nia. Kwa sisi inatubidi tuwe mfano kwanza kabla ya wananchi.”

Your work is going to fill a large part of your life, and the only way to be truly satisfied is to do what you believe is great work. And the only way to do great work is to love what you do. If you haven't found it yet, keep looking. Don't settle. As with all matters of the heart, you'll know when you find it.

Steve Jobs