Kanye West.
Kanye na Kim
New York, Marekani
MWANAMUZIKI nyota wa Marekani, Kanye West na mkewe, Kim Kardashian, jana walihudhuria ndoa ya bosi wao katika tasnia ya muziki, Steve Stoute, na kuwa kivutio kikubwa walipoingia katika ukumbi wa harusi wakiwa wameshikana. Kanye ambaye alikuwa amevalia nguo za rangi nyeusi na ambaye ni mara chache kutabasamu, hivi karibuni amekuwa akiachia tabasamu ‘kubwa’ baada ya kutangaza kwamba atagombea urais wa Marekani mwaka 2020.