Tuesday, October 13, 2015

Je,CCM Watakubali Matokeo Iwapo Watashindwa??.......Majibu Yote Yako Hapa


Moja kati ya kitendawili kigumu kwa vyama vya siasa nchini ni iwapo watakubali matokeo kama watashindwa katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, swali hilo limekutana na majibu ya CCM.

Akijibu swali hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba alisema kuwa chama hicho hakina wazo la kushindwa kwa kuwa uwezekano huo haupo.

“Tangu mwanzo, uwezekano wa kushindwa haujakuwapo na hatujawahi kufikiria kwamba tutashindwa kwa sababu hilo halipo akilini kutokana na idadi ya wanachama wa CCM na ubora wa Dkt. Magufuli,” alisema January.

Mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa aliulizwa swali hilo wakati akiongea na kituo cha runinga cha Citizen cha nchini Kenya.

“Siwezi kusema nitachukulia kama nimeshindwa hadi nitakapothibitishiwa kuwa kila kitu kimeenda sawa kama hakuna hujuma,” alisema  Lowassa  na  kuongeza.
  
 “Tunaogopa sana kuhusu hujuma, kila mtu unaeongea nae unapokutana nae anakwambia ‘utashinda, lakini je, watakubali kushindwa?”