Mwigizaji wa filamu mwenye umbo la Kiafrika zaidi, Kajala Masanja aliamua kuwatolea uvivu baadhi ya mashabiki wachache ambao walikuwa wakimshabulia kwa –comments kuwa picha hizi alizoziweka mtandaoni akiwa ufukweni, hazina maadili kwasababu amevaa nguo ambazo zinaonyesha sehemu kubwa ya mwili wake.
Baada ya mjadala wa picha zake kupamba moto huku wengine wakiona zipo sawa kwani akionekana wakila denda na mwanae na wachache wakisema kuwa hazina maadili, Kajala aliingilia kati na kufafanua kuwa picha hizo alipiga wakati akiwa ufukweni nasio yupo mitaani anatembea.