Monday, January 25, 2016

Baridi ilivyosababisha baadhi ya Viwanja vya ndege, barabara kufungwa Marekani…Video

Taifa la Marekani ni moja ya nchi zinazokumbwa na kiasi kikubwa cha baridi duniani.
Maeneo mengi Mashariki mwa marekani yamefukiwa na theluji kufuatia kuanguka kwa kiwango kikubwa zaidi cha theluji kuwahi kushuhudiwa.
Zaidi ya watu milioni 80 katika majimbo 18 wameathirika na theluji hiyo, pia usafiri wa reli,Barabara za magari na ndege umesimamishwa katika maeneo yote yaliyoathirika na zaidi ya watu 200,000 wamekumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme.
Maeneo mengine ya jiji la New York ambapo viwanja vyake vingi vimefungwa ukubwa wa theluji inafikia urefu wa mita moja.