Monday, January 25, 2016

Ujumbe wa Nick Cannon baada ya aliyekuwa mke wake Mariah Carey kuvalishwa pete ya uchumba..

Mume wa zamani wa mwanamuziki maarufu Marekani Mariah Carey, rapper na mchekeshaji Nick Cannon ameamua kutoa ya moyoni baada ya mkewe kuvishwa pete ya uchumba na mwanaume mwingine bilionea James Packer.
Cannon na Mariah Carey ambao walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha waliachana mwaka 2015 baada ya kutofautiana na kila mmoja kuendelea na mambo yake.
Mariah Carey aliingia kwenye uhusiano mwingine na bilionea James Packer raia wa Australia na sasa wameingia kwenye hatua nyingine ya uhusiano wao baada ya kuvalishana pete ya uchumba.
Nick Cannon hakuonyesha kuumizwa na uamuzi wa Mariah Carey na kuandika ujumbe ambao aliwapongeza wote kwa uamuzi waliofikia na kuwatakia muunganiko mwema katika maisha yao mapya

U