Monday, February 1, 2016

HAYA NDIO MAAMUZI YA MESSI KUHUSU HUYU MTOTO ALIYETENGENEZA JEZI YAKE KWA KUTUMIA MFUKO WA PLASTIKI NA KUIVAA

Wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu mtoto aliyetengeneza jezi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi kwa mfuko wa rambo na kuivaa. Kwa mapenzi ya dogo kwa Lionel Messi alitengeneza jezi yaArgentina yenye jina na namba ya Messi.
Picha ya dogo huyo mwenye umri wa miaka mitano iliingia kwenye headlines kati kati ya mwezi January na baaadhi ya vyombo vya habari kuanza kumtafuta, dogo anaitwa Murtaza Ahmadi anatokea Afghanistan maeneo ya vijijini, January 31 stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa taarifa zimemfikia Lionel Messi na anajiandaa kukutana na dogo huyo.
12
Stori hizo zinapata nguvu baada ya mtandao wa  Argentine Sports website TYC kuandika pia. Lionel Messi anatajwa kuamua kukutana na dogo, lakini bado haijajulikana tarehe wala muda.