Sunday, February 21, 2016

Mastaa waukacha msiba wa John Woka

wolker (10)
Mama mzazi wa ‘John Woka’ akiaga mwili wa mwanaye kanisani, katika hospitali ya Muhimbili.

 Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi, mastaa mbalimbali Bongo wameukacha msiba wa mkongwe wa Bongo Fleva, Michael Dennis ‘John Woka’ aliyefariki dunia Jumanne iliyopita baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi ya gari iliyokuwa kwenye matengenezo.
wolker (1)Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Ado Novemba (menye suluali nyeusi) pamoja na waombolezaji wengine wakiaga mwili wa marehemu.
Kitendo cha mastaa kutoonekana msibani kilijidhihirisha Jumatano iliyopita kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar, wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Woka uliosafirishwa kwenda jijini Tanga kwa ajili ya mazishi yaliyotarajiwa kufanyika katika Makaburi ya Sahare jijini humo.
wolker (8)Wakipakia mwili wa marehemu kwenye gari.
“Mmh! Hawa wasanii wa Bongo wana roho mbaya kwa kweli mbona leo hawapo hapa sitaki kuamini kama kuna mtu hamjui John Woka, hapa namuona H. Baba (Hamis Ramadhan), Sajenti (Husna Idd), Stara Thomas, Keisha (Khadija Shabani) na Ado Novemba wengine wote wameingia mitini kweli?” alihoji mmoja wa wafiwa.
wolker (9)
Baada ya kusikia dukuduku hilo, paparazi wetu alizungumza na H. Baba ambaye asema amechukizwa na kitendo cha mastaa wa muziki kutojitokeza msibani hapo na kusema kuwa, wengi wao wanapenda mauzo huenda walihisi siku hiyo hawatauza sura.
wolker (6)Msanii mkongwe wa bongo fleva, Mgosi Mkoloni (mwenye fulana nyekundu) akiaga pamoja na waombolezaji wengine katika kuuaga mwili wa marehemu.
“Walichokifanya siyo sawa kabisa wengine kazi yao ‘kupost’ mitandaoni msibani hawaji, lazima wakumbuke mauzo yote ya hapa duniani mwisho wa siku lazima kila mmoja arudi kwenye udongo, isitoshe jana haikuwa wikiendi kusema wamechoka na wala kipindi hiki hakuna shoo,” alisema H. Baba.wolker (7)
Naye msanii wa filamu Bongo, Husna Idd ‘Sajent’ alisema wasanii wengi walikuwa na taarifa, licha ya kusikia kwenye vyombo vya habari taarifa zilitumwa kwenye makundi yote ya wasanii.
wolker (2)Wakiwa kanisani
“Huu msiba umeniuma kweli, jamaa alikuwa mtu wangu wa karibu sana na hata kipindi cha nyuma niliwahi kuuza sura kwenye wimbo wake, nimeumia wasanii wenzangu kutofika katika msiba wake, kifupi hatuna umoja na tuna ubaguzi,” alisema ‘Sajent.’
wolker (4)Msanii wa bongo fleva, Hamis Ramadhan, “H-Baba”