Wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamezawadiwa magari ya kifahari baada ya kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani (CHAN).
Rais Joseph Kabila amemtunuku kila mchezaji gari gari la kifahari la thamani ya $60,000 (£40,000).Wachezaji hao pia wamepewa nishani.
- Wachezaji wa DR Congo walakiwa kishujaa
Mwandishi wa BBC Mbelechi Msochi anasema mchezaji Heritier Luvumbu Nzinga aliyeumia kwenye michuano hiyo pia ameahidiwa kwamba atasafirishwa ng'ambo kwa matibabu.