Staa wa bongo fleva Ali Kiba amekiri kuwa ushindani uliopo sasa kwenye muziki wa bongo fleva umemfanya arekebishe vitu kadhaa kwenye muziki wake hii ni pamoja na kufanya video zenye viwango zaidi.
Licha ya kauli yake hiyo Ali Kiba ameweka wazi kuwa ushindani haupo kabisa kwenye akili yake,yaani yeye hashindani na mtu yeyote yule.
“ushindani umenifanya nifanye marekebisho kwa mfano videos na support..Ushindani upo,ni kitu cha kawaida ila haupo akilini..naamini sishindani na mtu” alifunguka Kiba alipoulizwa anaonaje hali ya ushindani kwenye muziki wa bongo fleva.
Source: Clouds