Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa TMA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema maeneo yaliyotolewe taarifa za mvua za wastani, Juu ya wastani au chini ya wastani yataendelea kuwa hivyo japo uwezekano wa kuwepo jua upo kutokana na ongezeko la joto.
Dkt. Kijazi ameongeza kuwa Mamlaka hiyo itaendelea kutoa taarifa za hali ya hewa zenye uhakika na kusema utabiri wa msimu wa vuli mwaka jana,TMA ilitabiri kwa usahihi uliofikia kiwango cha asilimia 85.8.
Mkurugenzi huyo wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kutambua umuhimu wa TMA na kuboresha mashine za kufanyia utabiri na kuajiri wataalamu ambao kwa pamoja wanashirikiana kutumia mitambo ya kisasa kuufamisha umma.
Aidha, Dkt. Kijazi ameongeza kuwa wako katika mkakati wa kuongeza vitu vya hali ya hewa nchi nzima ambapo wataanza na Dar es Salaam ambako kuna vituo viwili tu huku mahitajia yakiwa ni vituo zaidi ya 10