Mama Diamond akifanya usafi kwenye nyumba yake ya Tandale hivi karibuni.
Mama wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake kwa kununua mtaa mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba yake aliyokuwa akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi milioni 100.
Diamond na Mama yake Sandra.
Chanzo chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’ huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia ujenzi sambamba na binti yake, Esma.
Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.
“Mama Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe wao,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimezidi kutiririka kuwa mama Diamond anataka kuifanya nyumba hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na kuiboresha, kuna mpango wa kutengenezwa swimming pool (bwana la kuogelea).
Ikiwa inakarabatiwa.
Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba hiyo na kuzungumza na mama Diamond aliyekuwa bize kusimamia ujenzi.
Baada ya kukarabatiwa.
“Jamani! Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu iwe bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda mje mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.