Sunday, March 13, 2016

STAR ALIKIBA AMFUNGUKIA MAZITO JOKATE, NA KUMBWAGA AZARANI


DAR ES SALAAM: Staa anayesumbua na wimbo wa Lupela, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amedaiwa kumlipua Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa kusema hakuwahi kuwa na mpango wa kudumu naye penzini, Risasi Jumamosi linakupa ubuyu kamili.

Hivi karibuni, Jokate alizungumza na wanahabari wa Global Publishers na kudai amemchoka mpenzi wake huyo hivyo ameamua kumuacha rasmi Kiba ambapo habari hiyo ilichapwa jana kwenye Gazeti la Ijumaa.

kiba jokateKiba na Jokate.
Chanzo kilicho karibu na Kiba kimeweka bayana kuwa mkali huyo hakuwa na mpango na penzi la Jokate lakini alilazimika kuwa naye karibu kwa shughuli za kikazi (muziki).
“Tunamshangaa Jokate kusema eti amemchoka Kiba leo wakati anajua kitambo tu Kiba hakuwa na mpango naye. Kiba alilazimika ‘ku-fake’ penzi kwa sababu walikuwa wanafanya kazi za pamoja, hakuwa na jinsi.

Jokate
“Jokate mwenyewe anajua kwamba Kiba hakuwa na mpango naye. Nafikiri kajitokeza kwenye ‘media’ ili aonekane yeye ndiyo kamuacha Kiba kumbe mwenzake hata hakuwa na mpango wa kuwa naye,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Kiba katika simu yake ambapo alidai hapendi sana kuanika mambo yake binafsi kwenye vyombo vya habari lakini mmoja wa mameneja wake aliyeomba hifadhi ya jina, alifafanua suala hilo.
“Kiba hakuwa na mpango na Jokate na ndiyo maana kila siku tunapokuwa kwenye kazi zetu hapendi umtajie ishu za Jokate hata kidogo na alikuwa akisisitiza kweli lakini sisi tulikuwa tunalazimisha waendelee kwa sababu tulikuwa tunafanya kazi za pamoja,” alisema meneja