Saturday, March 12, 2016

Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya(CHADEMA) Akamatwa na Polisi usiku wa Kuamkia leo Akiwa hotelini jijini Mwanza


Mbunge wa jimbo la Bunda,Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi  jijini Mwanza na kulazimika  kulala  rumande baada ya kunyimwa dhamana.

Polisi walivamia Hoteli aliyofikia mbunge huyo na kumkamata majira ya saa 7 usiku na kisha  kumpeleka  kituo cha kati cha Jijini Mwanza akiwa ameambatana na Mhe. Halima Mdee (Mb) , Joyce Sokombe (Mb) pamoja na Wakili John Malya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Justus Kamugisha amesema  hati ya kukamatwa kwake imetoka ofisi ya Bunge na kwamba Mbunge huyo anashikiliwa kama mtuhumiwa ambaye anatakiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.

Wabunge hawa pamoja  na  uongozi  wa  juu  wa  CHADEMA  Wako  jijini  Mwanza  kwa  ajili  ya  kikao  cha Baraza  Kuu  la  chama  hicho kinachofanyika leo katika Hotel ya Gold Crest