Thursday, March 24, 2016

Mtalaka wa Nora aitwa ‘Bushoke’

IMG-20160320-WA0027Akikrangiza.
DAR ES SALAAM: Makubwa! Mtalaka wa msanii mkongwe wa sinema za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’, Luqman Masoud amedaiwa kufanywa ‘mume bwege’ na mkewe wa sasa ikidaiwa kuwa anafanyishwa kazi za nyumbani kila siku.
Kutokana na kitendo hicho, imeelezwa kuwa baadhi ya ndugu wa Luqman wamefikia hatua ya kumuita mume bwege.
Chanzo makini ambacho ni ndugu na Luqman (kimeomba hifadhi ya jina), kimeeleza kuwa, mara nyingi ndugu yake huyo amekuwa akijishughulisha na kazi za nyumbani tofauti kabisa na wanaume wengine wanavyofanya mpaka kuna wakati aliwekwa kikao na majirani zake.
IMG-20160320-WA0058Akiandaa unga kwa ajili aya kupika Ugali.
Ndugu huyo alizidi kumwaga mchele kwa kueleza kuwa, kinachowakera zaidi wakati Luqman akiwa anafanya kazi hizo, mkewe mara nyingi anakuwa amelala au amekaa anasubiri chakula kiive ili ale na kupumzika hadi siku nyingine.
“Kwa kweli hakuna kitu kinachoniuma kama hicho kila nikienda kumtembelea ndugu yangu namkuta yupo jikoni anakuna nazi au anapika wali nachukiaga sana, tena sana na nikimwambia anakuwa mkali kupitiliza, sasa hivi ndugu wanamuita mume bwege,” kilisema chanzo.
IMG-20160320-WA0061Akiandaa tui la Nazi.
Amani lilifanikiwa ‘kumpandikiza’ mtu nyumbani hapo na kufanikiwa kunasa picha mbalimbali zinazomuonesha Luqman akiwa bize kushughulika na kazi za upishi.
Baada ya gazeti hili kunasa picha hizo, lilimtafuta Luqman kwa njia ya simu na kumuuliza anaipokeaje hali ya kuitwa mume bwege ndipo akasema amekuwa akifanya kazi hizo kutokana na ujauzito alionao mkewe wa sasa na si vinginevyo.MtalakaSiku ya ndoa yao.
“Mimi mke wangu kwa hivi sasa ni mjamzito ndiyo maana inakuwa hivyo na siwezi kuacha kumsaidia kwa sababu namuonea huruma hivyo namsaidia atakapokuwa sawa ataendelea na majukumu yake hao wanaosema mimi ni mume bwege waseme tu, sitawasikiliza kamwe hata majirani waniweke vikao vingapi,” alisema Luqman.
Luqman na Nora walifunga ndoa mwaka 2010 lakini wakaachana kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe.