Tuesday, March 29, 2016

Zitto Kabwe Atoa Ya Moyoni Baada Ya Serikali Ya Marekani Kusitisha Uhusiano Na Serikali Ya Tanzania Na Kuzuia Trilion 1 Kwenye Mradi Wa Umeme Vijijini Sababu Ikiwa Ni Zanzibar Na Cybercrime Act


 Serikali ya Marekani imesitisha mahusiano na Serikali ya Tanzania kwenye miradi ya MCC. Hivyo Tanzania itakosa jumla ya tshs 1trn ambazo zilikuwa zimeelekezwa kwenye Umeme na Umeme vijijini. Sababu? Zanzibar na Cybercrime Act. Siku si nyingi tutawasikia Umoja wa Ulaya nao. Nasubiri kusikia Serikali ya Rais Magufuli itasema nini. Suala la Zanzibar likitazamwa kibabe kwa kuwa watawala wana maguvu nchi itaingia kwenye matatizo makubwa sana ya ndani bila kujali misaada inakatwa au la. Sipendi misaada. Sipendi mataifa ya kigeni kuingilia masuala yetu ya ndani. Lakini Tanzania sio kisiwa, tunaishi ndani ya jamii ya kimataifa. Kuna mambo lazima tufanye kwa kuzingatia misingi ya kidunia. Zanzibar ni moja ya jambo hilo. Tusiweke kichwa kwenye mchanga kama mbuni.....
BY: ZITTO KABWE