Kigogo wa wema, Clement Kiondo ‘CK akiwa bize jikoni.
Upepo umebadilika! Aliyekuwa kigogo serikalini katika idara nyeti kabla ya ‘kutumbuliwa’ na kufikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar kwa tuhuma za kughushi hundi na kujichotea fedha kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye aliwahi kudaiwa kuwa mwandani wa staa wa Bongo, Wema Isaac Sepetu, Clement Kiondo ‘CK’ au Kigogo wa Wema amenaswa laivu akichoma na kuuza mishikaki.
RISASI JUMAMOSI LAPEWA ‘UBUYU’
Hivi karibuni, Gazeti la Risasi Jumamosi lilipokea simu kutoka kwa chanzo chake kikisema CK ziku hizi anauza mishikaki. Mazungumzo yalikuwa hivi…
Chanzo: “Haloo…naongea na Risasi Jumamosi hapo?”
Risasi Jumamosi: “Ndiyo…karibu, tukusaidie nini?”
Chanzo: “Hivi mna habari kuwa yule Kigogo wa Wema. Mnamuita CK, siku hizi anatuhudumia mishikaki baa?”

Risasi Jumamosi: “Lakini sisi hatuoni tatizo. Kwani ni yake au anamsaidia mtu? Na ni sehemu gani?”
Chanzo: “Hakuna tatizo lakini sasa amekuwa gumzo. Hebu fikirieni alivyokuwa na Wema na Kajala (Masanja) alikuwa anafanya makubwa lakini sasa anauza mishikaki na kuhudumia wateja kwenye pub. Ni hapa maeneo ya Leaders Club (Kinondoni) kwa mbele, nyuma ya Ubalozi wa Ufaransa.”
Risasi Jumamosi: “Tunashukuru kwa taarifa ndugu, tunakuahidi kuifanyia kazi kwani sisi kwetu ni ‘hapa kazi tu’.

Chanzo: “Tunawaamini kwa kufuatilia mambo. Unajua hawa vigogo wanaotumbuliwa na serikali kwa sasa wanatia huruma sana. Ukilinganisha maisha waliyokuwa nayo kabla ya kutumbuliwa na sasa, utawahurumia.”
…Akichoma mishikaki.
Risasi Jumamosi: “Ukiacha CK, hata hao vigogo wengine tunawafuatilia, endelea kusoma Magazeti Pendwa ya Global Publishers.”
Chanzo: “Tupo pamoja.”
Chanzo: “Tupo pamoja.”
RISASI JUMAMOSI LAMFUNGIA KAZI
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Jumanne ya Aprili 5, mwaka huu, Risasi Jumamosi lilituma ‘makachero’ wake kutoka kwenye kikosi maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kuitafuta grosari hiyo ili kuthibitisha kilichodaiwa.

MUDA WAKE KWA SIKU
Katika mazungumzo ya udadisi, OFM walibaini kuwa, CK hupatikana kwenye ‘pub’ hiyo mishale ya kuanzia mchana na kuendelea hadi usiku.

Siku hiyo, makachero wa OFM walitinga kwenye pub hiyo (jina tunalo) na kuhudumiwa mishikaki na soda lakini picha za CK hazikupatikana kwa vile kuliwa na giza na pia mwenyewe alionekana kuwa na machale hivyo makachero kuhofia namna ya kumnasa.
SIKU YA PILI
Aprili 6, mwaka huu, yaani Jumatano, Risasi Jumamosi lilibadilisha makachero ambapo lilituma wengine wenye mbinu kubwa na za kisasa za kunasa matukio.
Makachero hao walitia timu eneo hilo mishale ya saa kumi jioni na kutua kwenye pub hiyo ambapo walifanikiwa kumnasa laivu CK akiwa amesimama nje akiongea na simu.
Makacharo walitafuta sehemu nzuri ya kukaa ili iwe rahisi kumfotoa picha pale kazi itakapoanza. Wakati makachero wakikaa hapo, wengine walibaki ndani ya gari tayari kwa kuongeza nguvu endapo itatakiwa kuwa hivyo.

AONESHA WASIWASI KWA OFM
Hata hivyo, CK alionekana kuwa na wasiwasi na makachero wetu kwani muda mwingi aliwapiga chabo licha ya kwamba hakuwa akijua ni akina nani.

Ukaaji wake uliwasumbua sana makachero waliokaa kwenye pub hiyo hivyo kuwa vigumu kumpiga picha akiwa jikoni kwenye mishikaki. Ndipo kachero mmoja miongoni mwa waliobaki ndani ya gari, alipewa maelekezo na kamanda mkuu kwenda jikoni kununua mishikaki ili iwe rahisi kumpiga picha.
CK AMHUDUMIA KACHERO
Kachero wa OFM alitua jikoni na kuomba oda ya mishikaki minne kwa CK na mrembo mmoja aliyekuwemo humo ambapo walisema inapatikana.
Kachero: “Basi nifanyie.”

CK: “Vipi, uwekewe na pilipili au?”
Kachero: “Yeah! Yeah! Muhimu.”
CK aliachia tabasamu laini kuashiria ukarimu wake kwa wateja huku akiigeuzageuza mishikaki hiyo huku kachero akimfotoa picha za kumwaga. Baadaye alilipa pesa na kurudi kwenye gari.

MBALI NA MISHIKAKI
Mbali na kuuza mishikaki, pia CK alishuhudiwa akiwahudumia vinywaji wateja wake huku mara kwa mara akitoka nje ya eneo hilo na kuchungulia kisha kurudi ndani huku akizungumza kwa simu. Pia, wakati mwingine alitoka na baadhi ya wateja na kuzungumza nao nje kisha kurudi tena ndani.
Baada ya kukamilisha zoezi lao na kushiba mishikaki kisha kushushia na vinywaji, makachero walimuaga CK huku wakimuahidi kurudi siku nyingine kupata mishikaki.

…Alipofikishwa Mahakama ya Kisutu.
WEMA ADAIWA KUMKWEPA
Kuna madai kwamba, siku moja Wema aliwahi kufika kwenye pub hiyo kwa kuitwa na ‘zilipendwa’ wake huyo lakini alipofika hakushuka ndani ya gari zaidi ya salamu ya juu kwa juu na kuondoka zake.
MHARIRI NAYE
Picha za CK zilipofika mezani kwa mhariri, naye alifanya jitihada za kuzungumza na CK ili kujua nani mmiliki wa biashara hiyo kwani huenda ikawa anamshikia mtu lakini simu yake haikuwa hewani hivyo jitihada hizo zinaendelea.

YATOKANAYO
Kabla ya ‘kuharibu’ serikalini na kutumbuliwa, CK alidaiwa kumpangishia Wema nyumba ya kifahari Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, kumnunulia gari la bei mbaya aina ya Aud Q7 na kumfungulia Kampuni ya Endless Fame Productions iliyokuwa na ofisi zake maeneo ya Mwananyamala, Dar.

Baada ya CK kupata majanga, Wema alinyang’anywa gari hilo na jamaa aliyedai kuwa hakuwa amelipwa fedha zake.
Kwa upande wa ofisi, ilifungwa baada ya CK kuchukua vitu vyake vyote ikiwemo kompyuta, kamera na vifaa vingine kisha kurudisha nyumba kwa mmiliki wake kwa kile kilichodaiwa kuwa, ni Wema kuchepuka na Diamond.

Kuhusu nyumba, awali Wema alidai aliinunua lakini Magazeti ya Global yalifichua kuwa alikuwa amepangisha ambapo baadaye alishindwa kulipa umeme na maji hivyo kutimuliwa na mmiliki wake aliyetajwa kwa jina moja la Ngoma na kwenda kupanga Ununio jijini Dar.
Wema Sepetu
Katika sarakasi hizo, ilibainika pia kwamba, zile Sh. milioni 13 ambazo Wema alimlipia Kajala ili asiende jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano na mumewe Faraji Agustino (miaka 7), zilitoka kwa CK ambaye wakati huo alikuwa na fedha za ‘kumwaga’.
Kajala na mumewe, walihukumiwa kwa mashtaka matatu; kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar, kuhamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 na kutakatisha fedha kinyume cha sheria.
CK ALITAJWA KUWAGOMBANISHA WEMA, KAJALA
Hata hivyo, madai mengine yaliandikwa magazetini kuwa, CK ambaye alikuwa na mke wa ndoa, ndiye aliyewagombanisha Wema na Kajala baada ya kudaiwa kuwazunguka na kutoka nao jambo lililoibua uhasama baina ya warembo hao huku Kajala akioga shutuma zaidi kwa madai kuwa, alimkwapua shemeji yake.

NENO LA MHARIRI KWA CK
Pamoja na yote hayo, neno la mhariri kwa CK (kama biashara hiyo ni yako) ni kusimama imara ili uweze kwenda mbele. Usiruhusu kuchukuliwa muda kwa kuwaza maisha ya nyuma kwani kwa kufanya hivyo, kunaweza kukurudisha nyuma zaidi badala ya kusonga mbele.

GPL