Saturday, April 9, 2016

Shamsa amsweka lupango mzazi mwenziye

IMG_0006
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford.

STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford juzikati amemsweka lupango mzazi mwenziye Dick Matoke, katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa kile kinachodaiwa kuwa mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kumtukana mara kwa mara akishirikiana na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Dick na mwanamke wake wa sasa wamekuwa wakimtumia meseji za matusi Shamsa kitendo ambacho mwigizaji huyo alikuwa akikivumilia lakini katikati ya wiki hii, uvumilivu ukamshinda, akaamua kwenda kumshtaki.
“Yaani hakuna kitu ambacho Shamsa alikuwa hakipendi kama kutumiwa meseji na mzazi mwenzake huyo na mwanamke wake zikimtusi kwa maana alivumilia mpaka akachoka, akaona bora aende polisi kumshtaki,” kilisema chanzo.shamsaa900Shamsa Ford enzi akiwa na mzazi mwenziye Dick Matoke.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, baada ya kwenda polisi na kufungua mashtaka yaliyosomeka; OB/RB/6522/2016, usiku wa Aprili 6, mwaka huu, polisi walikwenda nyumbani kwa Dick maeneo ya Mikocheni jijini Dar ambapo walifanikiwa kumkuta, wakampeleka kituoni Oysterbay.
“Polisi wanaendelea kumtafuta na mpenzi wa Dick aliyekuwa akishirikiana naye kumtukana Shamsa ili naye waweze kumhoji kisha hatua nyingine za kisheria zichukue mkondo wake,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Shamsa kuhusiana na sakata hilo, alikiri kutokea lakini akaomba muda ili alizungumze vizuri kwa kile alichosema yuko  bize na shughuli zake za filamu.
“Mh! Umeipata hiyo na wewe?  Nani aliyekuambia? Any way ni kweli imetokea lakini nitakuelezea vizuri nikitulia, niko bize kidogo na kazi,” alisema Shamsa.