Msanii wa filamu nchini Riyama Ally ambaye siku za karibuni ametolewa mahali na msanii wa muziki wa kizazi kipya Leo Mysterio amevunja ukimya kwa watu ambao wamekuwa wakisema kuwa anatoka na dogodogo huyo.
Riyama amesema kuwa wanataka atoke na mzee ndiyo wamuone kuwa ana heshima.
Kupitia kipindi cha eNEWS kinachorushwa na EATV Riyama amesema kuwa Leo Mystereo ndiyo furaha yake, na ujio wake katikia maisha yake umemuongezea changamoto kwenye maisha yake na kumfanya awe na furaha muda wote.
” Watu wanatakiwa wajue penzi haliingiliwi wewe ukicheka au ukinuna mimi hainisaidii kwani mimi natafuta furaha yangu na huyu ndiye furaha yangu, wewe unataka mimi niondoe furaha yangu nitaipata wapi. Unataka niwe na babu wa miaka mingapi ili uone Riyama ana heshima huyo babu unayetaka niwe naye asiponiheshimu pia mtasema. Jamani binadamu kweli maneno yapo kwa ajili ya kusema ila inabidi tuwe tunachagua vitu vya kusema” alisema Riyama Ally.
Riyama alisema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea vibaya sana juu ya mahusiano yake lakini amewataka kutambua kuwa wao wamependana na wana mipango na wameridhiana wao hivyo kuwatenganisha kwa maneno si jambo jepesi.