Sunday, May 25, 2014

Hivi ndivyomilivyokua:Tapeli awaingiza mjini Chief Mareale na Mrisho Mpoto...SOMA ZAIDI


Binti mmoja wa kilokole hapa jijini Arusha amezua heka heka na gumzo baada ya kuwaingiza mjini aka kuwatapeli watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu maarufu kama vile Chief Mareale kutoka uchagani na msanii wa kughani ndugu Mrisho Mpoto.

Inasemekana nusura tego hili la kitaplo limkute mheshimiwa rais alipokuwa ziarani jijini Arusha wiki kama moja na ushee iliyopita.

Binti huyu aliyetumia mwamvuli wa 'bwana yesu asifiwe' aliandaa tamasha feki la kutangaza utamaduni ambalo lilitakiwa kuwajumusha machifu,watemi,maleigwanani,ma mwinyi na wakuu mbalimbali wa makabila ya Tanzania.Idea ilikuwa superb hata watu wa TANAPA walitaka kuidhamini na hata mheshimiwa rais angeombwa kufungua tamasha hili!

Hatimaye tamasha lilianza kwa maandamano tena yakishirikisha kina chief Mareale akiwa kapanda ngamia kama matajiri ya dubai yanavyobeba falcon!

Tamasha likaendelea na ilipofika siku ya kilele yaani jumamosi ndipo tafrani likaanza.

Binti wa kilokole ambaye ni director wa NGO feki akatokomea kusikofahamika na kuwaacha solemba wateja wa tamasha,waandaaji kwa maana ya wafanyakazi wake na wote waliokodishwa,kina Mrisho Mpoto na Mareale waliolala hoteli bila kulipiwa wala kulipwa.

Hatimaye jamaa zetu wa Fanya Fujo Uone wakavamia tamasha hapo uwanja wa shekh amri abedi ili kuepusha maafa yatokanayo na hasira za wote walioingizwa cha kike!

Kwa sasa binti huyu yuko nje kwa dhamana na inasemekana anadaiwa karibu shilingi milioni 80.