Sunday, May 25, 2014

Idadi ya Wanawake wanaoendesha Ndege, Treni, Malori na Mabasi Tanzania imetajwa na Wizara ya uchukuzi..WATAZAMA HAPA WANAWAKE HAO!!

airplaneNi mara chache sana tunapata takwimu kama hizi kutoka kwenye ngazi ya juu ya serikali ya Tanzania ndio maana hii stori imekua kubwa baada ya kutolewa na Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe bungeni Dodoma May 24 2014.
Waziri Mwakyembe amesema pamoja na ugumu wa kazi ya udereva Tanzania kuna madereva Wanawake watatu wa mabasi makubwa na Wanawake wawili wa malori ya mizigo kwenda Lubumbashi Congo.
Vilevile kuna Wahandisi Wanawake 15 wa mitambo kuongozea ndege, kuna Wanawake 8 madereva wa Treni, marubani 8 Wanawake, waongoza ndege 16 Wanawake.
Konda Mwanamke
Huyu ni mmoja kati ya Wanawake Makondakta kwenye jiji la Dar es salaam ambao niliowaona kwa macho yangu ni zaidi ya watatu.