Monday, June 2, 2014

TAARIFA RASMI YA POLISI JUU YA TUHUMA ZA UBAKAJI ZINAZOMKABILI MME WA FLORA MBASHA..SHUKA NAYO


Jeshi la Polisi limethibisha kupokea tuhuma za ubakaji dhidi ya mume wa mwimbaji wa injili Flora Mbasha anayefahamika kwa jina la Emmanuel Mbasha.

Akiongea na Tovuti ya Times Fm, kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi ameeleza kuwa jeshi hilo limepokea tuhuma hizo kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni binti mwenye umri wa miaka 17 na kwamba binti huyo alifika katika kituo cha polisi akiwa na ndugu zake.

“Taarifa zimepokelewa na zinachunguzwa. Taarifa zilizokuja ni za kubaka sasa tunazichunguza tufike mwisho tujue ni nini.” Kamanda Minangi ameimbia tovuti ya Times Fm.

Ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa mlalamikaji polisi walienda nyumbani kwake ambapo hawakumkuta yeye na mkewe na kwamba hadi sasa hawajapatikana.

Tovuti ya Times Fm ilitaka kupata ufafanuzi kuhusu uhusiano uliopo kati ya mlalamikaji na mtuhumiwa kwani taarifa za awali zinadai kuwa ni shemeji wa mtuhumiwa.

“Hayo yote yanachunguzwa, mimi siwezi kusema ni shemeji yake kabla hatujafikia mwisho wa uchunguzi. Tutakapofikia mwisho wa uchunguzi ndipo tutakapoweza kusema wana mahusiano gani.” Kamanda Minangi ameeleza.