Saturday, September 20, 2014

ABIRIA WASHIRIKI KULETA MAAFA YA AJALI NCHINI!!! WANABEBA VITANZI VYAO WENYEWE!

Abilia wakipanda baada ya basi kupimwa 
uzito kwenye mizani.
WAKATI serikali ikifanya kazi nzito ya kujenga barabara kwa gharama kubwa na kuzilinda kwa kuweka mizani ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito, baadhi ya madereva wa mabasi wamekuwa wakimpiga changa la macho Waziri wa Ujenzi, John Magufuli anayesimamia barabara nchini.
Madereva hao huzidisha abiria na hivyo basi kukosa sifa kwenye mizani wakati wa ukaguzi lakini wanachofanya sasa, kila wanapokaribia mizani hupunguza uzito kwa kuwashusha baadhi ya abiria nyuma ya mizani na baadaye kuwapakia  kwa mbele baada ya kupima.
Kubeba abiria kupita kiasi imekuwa ni chanjo mojawapo kikuu cha ajali za majini na nchi kavu!!!
Cha kusikitisha ni ushiriki wa abiria katika dhuluma hii ya uhai wao wenyewe!!!