Mdau mmoja mkubwa wa muziki duniani alipokuja Afrika aliwahi kuwaambia Watangazaji wa Radio ni kiasi gani ambavyo mastaa wa dunia wamekua wakilipwa pesa nyingi kupiga picha wakiwa watupu na kuzifanyia biashara kwa kuziuza mamilioni ya pesa kwenye Majarida pamoja na vyombo vingine vya habari.
Yani biashara imegeukia huko na akamtolea mfano Rihanna ambae aliwahi kupiga picha za namna hii na kulipwa mamilioni ya fedha za Kitanzania kwa sababu tu ya picha zake 7 za utupu zilizotumiwa.
Katika siku za karibuni taarifa kubwa ambazo zimetangazwa mpaka na vyombo vikubwa vya habari duniani ni kuhusu tatizo la kuvujishwa kwa picha za utupu za watu maarufu wakiwemo Waigizaji wa dunia kama Meagan Good na Gabrielle Union ambae alikuwepo Tanzania siku kadhaa zilizopita.
Kibaya zaidi kilichofanya wengi wamlaumu ni baada ya kujulikana kwamba picha hizi alizisambaza kwa makusudi na sio kama kisingizio cha wengine kwamba wamepoteza simu au kuibiwa.