Saturday, September 20, 2014

ANGALIA HAPA VIDEO JINSI WAANDISHI WA HABARI WALIVYOSHUSHIWA KIPIGO NA POLISI


Siku moja baada ya makamu wa rais Dkt Mohamed Ghalib bila kuhimiza mahusiano mema wakati wa utendaji kazi baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na vyombo vya habari ,jeshi la polisi likiwa na silaha pamoja na mbwa limekiuka kauli hiyo kwa kuwapiga na kuwajeruhi baadhi ya waandishi wa habari na kuwazuia kutekeleza wajibu wao wakati mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema alipowasili katika makao makuu ya jeshi hilo kwa mahojiano.
Kivumbi hicho kilitokana na Jeshi la Polisi kutaka kuzuia maandamano yaliyotangazwa na Chadema mikoa yote nchini bila kikomo kwa lengo la kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalum la Katiba (BMK)