Thursday, September 4, 2014

DOGO MFAUME ADAIWA KUMTELEKEZA MAMA’KE

STAA wa muziki wa Mnanda Bongo aliyewahi kutamba na Wimbo wa Kazi ya Dukani, Dogo Mfaume (pichani chini)anadaiwa kumtelekeza mama yake mzazi, Flora Nathaniel (60), mkazi wa Chanika, Ilala jijini Dar ambaye amekatwa miguu kufuatia kukumbwa na ugonjwa wa Kisukari mwaka 2011. 
Staa wa muziki wa Mnanda Bongo aliyewahi kutamba na Wimbo wa Kazi ya Dukani, Dogo Mfaume.
Kwa mujibu wa majirani, mwanamke huyo aliyewahi kuwa nesi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa miaka 26, amekuwa akiishi kwa shida kufuatia ulemavu alionao lakini mtoto wake ambaye ni Dogo Mfaume hajali, haendi kumwona wala kujua nini kinaendelea.
 Dogo Mfaume alipotafutwa kuulizwa kuhusu hali hiyo alisema: ”Kusema ukweli uwezo sina, hali ya mama inaniumiza kichwa lakini  si kwamba nimemtelekeza bali nashindwa. Watu wenye uwezo wanaoguswa na hali ya mama wajitokeze kumsaidia.”
 Masaibu ya mama huyo yaliandikwa kwa undani kwenye Gazeti la Uwazi ambalo ni ndugu na hili Toleo la Agosti 26-Septemba Mosi, mwaka huu akimwomba Rais Kikwete na Watanzania wamsaidie kwani maisha yake ni magumu. Aliomba msaada upitie kwenye namba ya simu 0755 216 865.